Kilio chanisakama, nikimkumbuka maria

Mtoto hakika mwema, wengi walimsifia

Akamtenda unyama maria akajifia

Twakuomba e manani mlaze pema maria

 

Mtoto kichanga kweli chuchu nazo zachomoza

Miaka kumi kamili na maisha ya mwaangaza

Kumbe wana kampeni mwataka kumbagaza

Twakuomba e manani mlaze pema maria

Nakumbuka siku hiyo ya majonzi fokofoko

Furaha ilijaa mno vifijo huku na kule

Maria akacheka mno hakuwa na angaiko

Twakuomba e maanani mlaze pema maria

 

Saa kumi keshafika jioni yakaribia

Mama yake kakumbuka mafuta ya kupikia

Maria akainuka haraka kukimbilia

Twakuomba e  maanane  mlaze pema maria

 

Na mbio zake maria zikawa za sakafuni

Nyuma yake kafwatia jitu nene maunguni

Simama likamwambia na kumshika mkononi

Twakuomba e maanani mlaze pema maria

 

Kaburuzwa kichakani na kingwa akafungiwa

Akasakamwa mchangani na mikono kafungiwa

Akasakamwa kooni na ndipo kanajisiwa

Twakuomba e maanani mlaze pema maria

 

Mradi kishatosheka jisu likalichomoza

Shingoni alichoka kooni kapasuliwa

Damu ilitiririka bila shia kajifia

Twakuomba e maanani mlaze pema maria

 

Sheria ziwe imara kulinda wana wa kike

Wabakaji kuwadara gerezani wafungike

Watiwe pingu imara wakike tusalimike

Twakuomba e maanani mlaze pema maria

 

Hadi tamati watama machozi yanimwaika

Kifikiri wangu wana hawana wakuwashika

Twakuomba maulana uwape wakuwashika

Twakuomba e maanani mlaze pema maria

 


 

Ubakaji

Na: 

Elvinah Tatu Mohammed  (SHULE YA UPILI YA KWALE GIRLS)

Katika Ukumbi wa Kenya Heritage Training Institute  (KHTI)

3RD AND 4TH MARCH, 2016

Add comment


Security code
Refresh