MOHAMED MURSHID MUKHTAR

 

Naanza yangu kauli, salamu nawajulia,

Nikiwaomba mutuli, ili muweze sikia,

Kwa kweli siwezi tuli, mwana wa Tima nanena,

Karibu sana wazazi, shangazi baba na mama.

 

Shikamoo wangu mama, salamu nakujulia.

Nakumisi tena san, kila siku ya dunia,

nakupenda wako mwana, moyoni mi naumia.

Namuomba ya rabana, uishi miaka mia.

 

Sengine nakaa chini, nalia kwa machungu,

Ukifa sitaongea mimi, nitakuwa kama bubu,

Utayakata yangu maini, nitakuwa kama zuzu,

Ati waenda zikwa chini, waenda liwa na wadudu.

 

Miezi tisa kamili, menibeba matumboni,

Kijidogo changu mwili mekileta dunia usoni,

Miaka mengine miwili, waninnwesha maziwa bila warning,

Wanipa maziwa mara mbili, usiku night na morning.

 

Simu nakupigia, nikitaka pocket money,

Huninyimi wanipea, ili mwanao niwe faini,

Mpaka tripu wanilipia, nifurahike nite funney

Mbele  za watu nakuambia, I love u sana my mummy.

 

Unanipeleka na Uner, mpaka hospitalini,

Moyo wako unadunda, nipokuwa taabani

Mbinu nyingi unaunda, nisingie mashakani

Runda nitakujengea nyumba, nikifaulu masomoni

 

Mama leo nakuahidi, natia bidii masomoni,

Michezo weka baidi, kutia bidii sikomi,

Sitokuwa mkaidi, nitaupita mtihani,

Sitovuta bangi na widi, nitakufaidi wangu honey.

 

Wali wako ukipika, wachagua mchele wa sunrisi,

Utamu wake ni hakika, kichanganya na tui la nazi,

Chapati zako zina wika, sisemi mahamri na mbaazi,

Sina la kukulipa, mimi leo weka wazi.

 

Nitakubeba na bugatti, na watu hutogongana,

Utakuwa kati kati, na mahasidi hutozozana,

Tutaonana Augasti, kwaheri ya kuonana,

 

Naenda fanya mocki, Goodbye wangu mama

MASHAIRI NA MOHAMED MURSHID MUKHTAR UPPER HILL SCHOOL NAIROBI FORM 4 - 17 YEARS

Add comment


Security code
Refresh