Elimu hino elimu, jamani mbona twapu’za

Ma’rifa yalo muhimu, yatupasa kutukuza

Walimu twawashtumu, wavyele hawakubeza,

Elimu haina mwisho, bora bidii kufanya

 

Elimu ni ufunguo, sote hilo twaliJua,

Hekima ni ufunuo, na tamu kama halua,

Hi elimu ufufuo, hutupatia satua

Elimu haina mwisho, bora bidii kufanya

 

Mbona kuvunja sheria?dawa kuingiza shule

Tena bado fikiria, kupiga mtindi kule,

Fukuzwapo hususia, mbaya mwalimu Yule,

Elimu haina mwisho, bora bidii kufanya

 

Mboni zetu zaona, kwa walokosa elimu,

Wazurura kila kona, hawana kazi muhimu,

Lakini kwanini mbona, kwani elimu ni ngumu?

Elimu haina mwisho, bora bidii kufanya

 

Tamati sasa hakoma, mwenye sikio sikia

Sina neno limegoma, shapata wangu wasia,

Ukipenda mchongoma, kitu gani tarajia?

Elimu haina mwisho, bora bidii kufanya

 

 

NA

 

JINDWA DAVID CHIPURU

KATIKA UKUMBI WA KENYA HERITAGE TRAINING INSTITUTE (KHTI) 3RD & 4TH MARCH, 2016.

 

Add comment


Security code
Refresh

Highlights

Visitor Counter

2.png6.png0.png9.png4.png3.png
Today216
Yesterday472
This week688
This month8487
Total260943

Who Is Online

3
Online

Share This

Follow Us

Our Partners