Lakini kabla ya ya kuja ibn Batuta watu hao walikuwa wakiitwa wangozi, kutokana na mapokezi ya wazee wa kale wa Mombasa (Mfunzi) ni kua watu hawa walikuwa wakipima mashamba kwa vipande vya ngozi.  Kasha jina hilo likabadilika na kuitwa wavisai ama wakisai kwa kuwa walikuwa ni watu wakutoa visa na mwisho ndiyo kuitwa Waswahili.  Lifwatalo ni shairi la kingozi limetungwa na Ustadh Ahmad Juma Bhalo (Ustadh Bhalo)

Mwanzimle mlekele, ni mwina wa bangu moyo
Moyo mtipi wa male, yasofupika maziyo
Maziyo maku si mbale, maningayo sifumbile
Siyo ndmi si nga soyo, maningayo simbile
(Taa ya Umalenga u.k 22)

Licha ya Waswahili kuwa wenyeji wa kitambo kuliko makabila mengine kwa mwenye kuelewa tarekhe (histria) vizuri.  Kinachosikitisha na kushangaza ni kwamba kuwa lugha hii tukufu nay a kale ni ya kigeni,  yaani asili yake si Afrika.  Wanao shika kani (kulitiliya nguvu jambo) na kulipigiya upatu suala hilo si rahisi kutamka fikra zao, kwa kucheleya kuthibitisha kuwa ni wajinga wa histria ingawa Kiswahili kimethibitishwa kuwa ni lugha asili ya kiafrika bila kusaza shaka yoyote.

Kuna na wenye fikra ya kuwa utamaduni wa Kiswahili ni wa kigeni, na kupinga kuwepo kwa watu waitwao waswahili kwa kusingizia kuwa maneno ya Kiswahili mangi (mengi) yamefanana na kiarabu.  Dai hilo tukilipima vizuri tutaona halina mashiko maana takriban lugha zote ulimwenguni zimeazimana maneno. Kwa mfano hebu tutizame kiingereza kilivyoazima maneno kutoka lugha ya Kiarabu. Na maneno yenyewe ni kama yafwatayo;

1.    Amber              (anbar)
2.    Crimson           (Karmazi)
3.    Elixir                  (ikseer)
4.    Carat                (Kirat)
5.    Cotton              (al-Kutn)
6.    Sherbet             (Sharabat)
7.    Tahini                (tahina)
8.    Clipher    /zero     (sifr)
9.    Mask/mascra       (mascara)
10.    Alcohol               (al-kohool)
11.    Hazard               (zahr)
12.    Caliber               (kaleb)
13.    Jar                      (Ka’leb)
14.    Jar                      (jarra)

BASI KWANINI KIZUNGU KISIAMBIWE NI KIARABU LAKINI KISWAHILI KUWA NI KIARABU?
Na ale wanaokubali kuwepo kwa waswahili hutiya ila na kusema ati si kabila safi, na imetanganya (imechanganya) yaani kuambiwa Kiswahili ni lugha ya kigeni hapa Afrika mashariki. Madai haya yalizuka tu baada ya Africa kutawaliwa na waingereza, maana kabla ya ukoloni hapakuwako na shaka yoyote juu ya kuwepo kwa waswahili, wala lugha yao wala utamaduni wao.

Tete hizi za tuhuma za waswahili zilianza kuwashwa wakati wa ukoloni wa kiingereza, na zikabiririka zaidi pale nchi za Afrika mashariki zilipokaribia kuwa huru.  Kwa mfano wazungu walikuwa hawakubali kuwa mwafrika ana ustaarabu au jambo lolote la kuweza kuonyesha ulimwengu umiliki wa jambo Fulani. Ndipo leo tukaambiwa kuwa miji ya Kiswahili ni ya kiarabu kwa ajili ya milango yaliotongwa (chongwa) kwa nakshi za kupendeza, mavazi, majumba na kadhalika lakini ukiwauliza mambo haya yanatoka wapi sehemu za Arabuni hakuna awezaye kukujibu.

Marejeo:
Shihabudin Chiragdin na Mathias Mnyapala -  Historia ya Kiswahili.
Ahmad Nassir Juma Bhalo - Taa ya Umalenga
Shihabudin Chiragdin -    Kiswahili tokea ubantu hadi ki – standard Swahili
John Ayto - Dictionary of foreign words in English
Shihabudin Chiragdin - Kiswahili na wenyewe


Prepared by
Najeeb Ahmad Nassir Juma Bhalo
Cell No.      0729-906-761
E-mail        This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. 

Add comment


Security code
Refresh

Highlights

Visitor Counter

2.png6.png2.png7.png3.png9.png
Today145
Yesterday459
This week2484
This month10283
Total262739

Who Is Online

2
Online

Share This

Follow Us

Our Partners