Mihadarati jamani, shauri hili si geni

Tunaingia shimoni, mengi maswali bongoni,

Wasafirishao nani? Si kokeni si afyuni,

Maisha twapelekapi? Hebu tubadilisheni

 

Anza viongozi wetu, wavaa kondoo ngozi,

Wa badhiri mali yetu, kombo laenda jahazi

Zimefungwa mboni zetu hatuoni tona chozi

Maisha twapelekapi? Hebu tubadilisheni

 

Mihadarati twauziwa, twakengameka moyoni,

Wengi wawekwa watawa, zitumalize maini,

Kwetu wazidi wagonjwa, wamefika hatarini

Maisha twapelekapi, hebu tubadilisheni,

 

Tuondoe janga hili, la mihadarati Kenya,

Kwa manufaa kamili, sote bidii kufanya,

Taka ngoa jifya hili, uwe na hisia chanya,

Maisha twapelekapi? Hebu tubadilisheni

 

Shime jamanini , shime, usisite fanya hima,

Tujibidishe kiume, tusiwe na neno kama,

Meno sheria  yauma, tusiuze dawa jama,

Maisha twapelekapi? Hebu tubadilikeni

 

Na

Jindwa David Chipuru (ST Georges Secondary School, Mombasa)

Katika Ukumbi wa Kenya Heritage Training Institute  (KHTI)

3RD AND 4TH MARCH, 2016

 

 

Add comment


Security code
Refresh

Highlights

Visitor Counter

2.png6.png0.png9.png4.png3.png
Today216
Yesterday472
This week688
This month8487
Total260943

Who Is Online

3
Online

Share This

Follow Us

Our Partners