Kasha langu la zamani, kasha lisilo tumbuu

Kitasa ndani kwa ndani, naufunguo ni huu

Alofunguwa n’nani, amelivunda  maguu

 

Kasha muundo wa kale, simuundo waki sasa

 ni kazi ya watu wale,  sidhanie ni mambasa

Usifanye makelele, nimelipa mengi mapesa

 

Mafundi wote wa kale, kwa hivi sasa hakuna

Na walobaki wafile, kabisa hutawaona

Ilo baki ni vulele, na kazi sijaiona

 

Kasha la mkafuu, madhubuti sawa sawa

Lenye harufu ya fuu, kula ukilifungua

La nukia karafuu, na waridi usotiwa


 

Kasha Langu

Na

Khatib Mtenzi

Kutoka Shule Ya Upili Ya St Goerges High

Katika

Ukumbi Wa Kenya Heritage Training Institute (Khti)

 

3rd March, 2016

 

Add comment


Security code
Refresh

Highlights

Visitor Counter

2.png6.png0.png9.png4.png3.png
Today216
Yesterday472
This week688
This month8487
Total260943

Who Is Online

3
Online

Share This

Follow Us

Our Partners